wabeba lawama sehemu ya 8



Aliendelea kupanda juu zaidi huku akiwaacha mdomo wazi vijana hao. Aliyafikia na kuanza kuyachuma na aliyalusha chini vijana wamsaidie kuyaokota basi zoezi la binti SARAFINA lilimaliza kwa mda mchache huku kila mmoja wa vijana hawakuamini walicho kiona walihisi binti SARAFINA alishushwa na mungu tu kwani alikuwa mzuri hatari na mitego aliyokuwa akiwatega aliwapa shida sana vijana hao. Alishuka chini binti SARAFINA na kuwaambia vijana hao Leo atawapikia chakula cha jioni huku akichanganya na hivyo alivyo toa kwenye mti basi kila mmoja alingoja jioni ifike ili wale chakula cha binti SARAFINA. MWAKIPALE naye hakuwa mbali na binti SARAFINA kwani naye aliingiwa na (jini mahaba) kwani alimlia tageti kila kukicha.
Jua lilianza kufifiaa ndipo Kijana MWAKIPALE na vijana wawili walielekea walipo tega mitego yao. Walifika na kuvuna walichopanda kwa siku hiyo kiukweli kila kukicha walikuwa wanaongeza idadi ya kuvua samaki Leo walipata wengi kupita kiasi. Walitoa mitego yao na walipeleka kuuza samaki hizo na siku hiyo walijua tu wanaenda kula chakula cha binti SARAFINA basi waliuza sana walinunua vitu vingine ili watakapo jumuika kula chakula basi waongezee na hivyo walivyo nunua. Huku nyumbani walimwacha binti SARAFINA pamoja na Kijana (KABILO) ili wasaidizane kazib na binti yule kiukweli yule Kijana alisaidia licha ya kumtamani tamani binti SARAFINA alipokuwa akipika naye binti alikuwa akimtega vilivyo KABILO naye akufanya Kazi alibaki anadondosha mate tu. Vijana waliludi nyumba wakiwa wamesheheni vyakula vingi na vinywaji walifika na walikuta kila kitu kiko poa.
WABEBA LAWAMA

Chapisha Maoni

0 Maoni