Alijilusha ndani ya maji na kuanza kupiga kelele vijana wale walimshanga na kuwaza nani ataruka kwenda kumsaidia. Lakini Kijana MWAKIPALE alifahamu fika binti SARAFINA alikuwa anawajaribu tu licha ya binti yule kuonekana kama kazidiwa huku akiitaji msaada NAYE akujali ya nyuma akifikiria kweli binti ataweza kufa huku wakimwona naye aliluka ndani ya maji ili amuokoe chakushangaza binti SARAFINA alivyomwona tu Kijana MWAKIPALE akimsogelea naye kwa mbwembwe alionesha kama yuko fiti akuwa na shida yoyote. Vijana walishangaa sana kuona binti SARAFINA akiogelea kama kazaliwa kwenye maji vile. Basi Kijana MWAKIPALE akacheza naye kwenye maji ndani ya dakika chache na walipanda kwenye chombo na kuendelea na safari mapaka nchi kavu ili wasubirie jioni wakavune walicho kipanda kwa siku hiyo.
Walifika nchi kavu huku vijana wenzake na MWAKIPALE walianza kumtania sana huku wakimcheka kwani binti yule alionesha ustadi mzuri wa kuogerea kumshida yeye. Huku wakiendelea na matani yale binti SARAFINA aliwachomoka na kupanda juu ya mnazi ili atungue (kuchuma) tunda lililo iva kwa manjonjo na mitego mingi kwa vijana wale alipanda kwa mapozi huku akitupa macho kwa Kijana MWAKIPALE kwani alitokea kumpenda sana Kijana yule. Vijana walivyo mwona binti SARAFINA akiwa anapanda mti ule walisogea na kuangalia asije kuanguka bule. Basi walisogea kwenye mti huo na kumtazama binti SARAFINA huku kila mmoja akitoa macho bila ya kupoteza hata sekunde kushusha macho chini walizidi kumshanga binti SARAFINA kwani alizidi kuwaingiza majaribuni vijana hao "huku akiwa na lake jambo"
🎩🎩🎩🎩🎩🎩🎩🎩🎩🎓🛎🛎🛎🛎🛎🛎🛎🛎WABEBA LAWAMA
🎩🎩🎩🎩🎩🎩🎩🎩🎩🎓🛎🛎🛎🛎🛎🛎🛎🛎WABEBA LAWAMA
0 Maoni