Katika kijiji cha MFUNDI kilionekana sana kuwa na vijana Wapenda maendeleo ya kijiji chao na kilipelekea kuwa kijiji cha kwanza huku kikifatiwa na kijiji cha jirani kijulikanacho KWA jina la MWANDELO. Basi sifa za kijiji hicho zilienea kona na kona za vijiji vingine wazee walifurai sana KWA vijana wao kuonyesha maendeleo hayo. Walitokea vijana wanne huku wakiongozwa na rafiki yao MWAKIPALE huku wakifikilia wa tumie njia gani ili wapate Mali na fedha za kutosha na mahitaji yao lakini Kijana MWAKIPALE aliwafumbua vijana wenzie macho na kuwaambia hicho kipindi ni cha samaki wengi hivyo inabidi wa tumie nafasi hiyo ili watoke kimaisha" vijana wenzake walimuunga mkono na wakakubaliana kufanya hivyo. Waliaga familia zao na kuanza safari ya kwenda kuvua samaki
Walionekana wenye Furaha kwani wazo alilotoa Kijana MWAKIPALE liliwafika na kulielewa sana. Walifika kwenye bahari ya KATOROMO na kuanza na kutengeneza chombo ambacho kitawasaidia kwenye Kazi yao. Siku hiyo walitumia kutengeneza chombo na kusoma mazingira ya pale basi usiku ukafika na walilala huku wakiwaza kesho yake ndiyo Kazi itaanza. Asubuhi ilifika na kila mmoja wao aliamka na kupanda chombo kuelekea ambapo samaki walipokuwepo huku wakiamini watatimiza tu malengo yao. Walifika na kushusha mitego na kusubili mda ili waangalie walichoingiza KWA siku hyo lakini chakushangaza mda ukafika........
0 Maoni