Jinsi Ya Kuzungumza Na Mwanamke Ili Umvutie





Kama unatabia ya kushindwa ama kupata tatizo la kuongea na wanawake ambao wanakuvutia, basi ni wakati murua wa kwako kutafuta mbinu ambayo itakufanya wewe kuwa na ari na kutokuwa na wasiwasi wowote wakati ambapo unaongea nao.
Wakati mwingine, wanaume hujiskia ndivyo sivyo wakati wanapoongea na wanawake na mara nyingi wanapalia kutoongea na wao kabisa kwa sababu ya kujiskia ndivyo sivyo. Hii mwishowe inachangia kwa wao kutoweza kuwafahamu wanawake vizuri ama kushindwa kuwatoa date. Kama umechoshwa na jambo hili ambalo linakuandama siku nenda siku rudi, basi unahitaji njia rahisi ya kukuwezesha wewe kuzungumza na wanawake na kuyafanya maisha yako rahisi. Kama kumtoa mwanamke date sahizi ni jambo gumu kwako, basi unafaa kujua kuwa hilo halifai kuwa tatizo lako kamwe tena.

Hii hapa ndio njia rahisi ya kuongea na mwanamke ambayo itakusaidia kupata ujuzi kadri muda unaposongea.

1. Usijaze mazungumzo yenu na kwa kumsifu saana.
Kuna makumi ya wanaume katika nyanja hii ambao wanapenda sana kutumia maneno ya kumsifu mwanamke kama wameishiwa na maneno wakati wanapoongea na mwanamke. Wanaume wengine hufanya hivyo ili kudhihirisha kwa mwanamke kuwa wamevutiwa nao. Lakini makosa ni kuwa, kutumia maneno ya kumsifu mwanamke hayaongezi sana wala hayafanyi mengi kumsaidia mwanamke. Kwa hivyo, weka maneno ya kusifu kando, na uanze kuongea mambo mengine ambayo yatamvutia pia. Kama hutafanya lolote kando na kumwambia kuwa umemzimia kwa urembo wake au macho yake, utakuwa umejiweka level moja na wanaume wengine ambao wanatumia mitindo io kwa hio.
Kumbuka: wewe unawezekana kuwa si mwanaume wa kwanza ambaye umevutiwa naye. Mwanzo, kuna uwezekano mkubwa kuwa wanaume wote wanamuona yeye anavutia. Hii inamaanisha kuwa kumsifu wewe kwake haitakuwa jambo geni kwake.

2. Usijikite sana kuonyesha ya kuwa unamwona yeye anavutia
Kusistiza, ni kuwa haufai kuweka akili yako ijikite kuwa unamwona mwanamke unayeongea naye anavutia kupindukia. Ukijisahau tu ukianza kumfikiria vile ana urembo na kuvutia, utakuwa unajipa presha ambayo haitakuwa na manufaa yeyote kwa mazungumzo yenu. Kuna njia rahisi ya kuepuka jambo hili, ni kuwa unafaa kuidanganya akili yako kuwa huyo mwanamke unayeongea naye hana urembo wowote ule. Presha ikishuka katika mwili wako, utajiona umepata fursa rahisi ya kuweza kujieleza ukiwa pamoja na mwanamke yeyote yule.

3. Tafuta mambo ambayo munagawa kimaisha
Ok, haitakuwa jambo gumu vile mkianza kuongea mambo ambayo mnagawa ama intrest ambazo mnashare. Mwanzo kama mtaanza kuongea mambo ambayo mnagawa katika maisha, itakuwa ni njia rahisi ya wewe kuweza kupata namba yake ya simu ili kuweza kumshawishi kumtoa date.
Kumbuka: mwanamke akigundua kuwa mnashare intrest pamoja, hapo hapo atataka kuutumia muda wake zaidi mkiwa pamoja ili mpate kuzungumza intrest mnazoshare. Hivyo basi, fanya utafiti wa kina na ujaribu kuvumbua jinsi na njia utakayoitumia ili muweze kujumuika pamoja.

Chapisha Maoni

1 Maoni