Jinsi Ya Kumuuliza Mwanamke Umtoe 'Out'

Kila mwanamke huwa tofauti na mwingine. Hivyo huwezi kutumia mbinu moja kumuuliza mwanamke kumtoa out halafu ukafanikiwa kwa kutumia mbinu io hio kwa mwanamke mwingine. Kujua mahusiano na mwanamke ni jambo muhimu. Mfano hauwezi kuongea na mwanamke mgeni usie mfahamu sawia na mwanamke ambaye ni rafiki yako.




Kwa sababu hauwezi kujua ni wakati gani ama sehemu ipi unaweza kukutana na mwanamke uliyemzimia, nimeamua kuorodhesha kategoria tano kuu za wanawake ambao ukipatana nao inaweza kuwa rahisi kwako kuwauliza kuwatoa out kwa kutumia mbinu tofauti tofauti.

1. Kumuuliza kumtoa out mwanamke mgeni usiyemfahamu
Kumuuliza mwanamke usiyemjua mtoke out kwa mara ya kwanza inaweza kuonekana jambo gumu, haswa iwapo kama hauna stimu zozote kwa akili. Lakini ukikaa kwa umakini na kufikiria utagundua ya kuwa kutaka kumtoa out mwanamke kama huyu ni jambo rahisi kuliko yote.
Mwanzo kuna dhana tatu hapa. Kwanza ni kuwa ukienda kuongea na yeye una asilimia 50 kwa wewe kukubaliwa na asilimia nyingine 50 ya kukataliwa. Pia kuna asilia 100 ya kukataliwa iwapo hautachukua hatua ya kumuapproach na kumuuliza. So hapa sioni tatizo lolote. Unafaa ujaribu hio asilimia 50 kama iwapo atakukubali.

Jambo la kufanya: Usipoteze nafasi kama hii, jiamini na umuapproach. Msifie ya kuwa umekuwa ukimuangalia kwa masaa na umeshindwa kujizuia kumuangalia so ungelijutia iwapo hukuongea naye. Kumuuliza iwapo wiki inayokuja kama anaweza kuwa na wewe ili mwende kwa mkahawa flani inaweza kufanya maajabu. 
Pia unaweza kuchukua hatua ya kuomba namba kutoka kwake kiurahisi.

2. Kumuuliza kumtoa out mwanamke katika kilabu, mkawaha ama baa
Umekutana na huyu mwanamke katika klabu, house party, rave ama baa mkajiinjoy kwa kujibugia vileo, mkadengua maungo, mkafanya na mengine mengi lakini baada ya hapo umeamua ya kuwa unataka kumtoa mwanamke kama huyu deti. Uko na namba yake lakini unaogopa kuleta hali ya aibu kati yenu. Ni rahisi.

Jambo la kufanya: Mtumie jumbe isiyodhuru kwa kumwambia ya kuwa ule wakati ulikuwa naye ilikuwa siku ya ajabu na uliipenda. Mara nyingi atakurudishia meseji ya kukujibu hivyo hivyo. Ngojea hadi baada ya siku moja au mbili halafu umpigie simu. Mpigie simu na wala usimtext. Mwambie ya kuwa unataka kumjua zaidi kumhusu. Hatua hii itamshika kama saprize na hatajizuia kukataa ombi lako. Iwapo ushawahi kumbusu, kumpeleka kwa mkahawaha hakutatosha, kumpeleka lunch ni jambo muhimu zaidi.

3. Kumuuliza kumtoa out mwanamke unayesoma naye, rafiki wa rafiki yako, mwanamke unaefanya naye kazi
Huyu anaweza kuwa rafiki wa rafiki, mwanamke unayesoma naye katika darasa la sosholojia, ama mwanamke unayefanya yake katika ofisi moja. Well, hapa ndipo tatizo linatokea na hapa. Iwapo atakukataa lazima utakuwa ukiwa na yeye sehemu moja so hapa ni kujitahidi asikukatae.

Jambo la kufanya: Kuhepa situation ambayo inaweza kuleta mushkili hapa, lile la kufanya ni kuanza na hatua ambazo haziwezi kudhuru. Muulize ile siku ambayo atakuwa yupo free na umualike katika sehemu flani uliyoizoea. Hapa matumizi ya vileo inapendekezwa zaidi kuliko kawaha. Hakikisha mnakunywa chupa moja mbili ili kutoa tenshen yeyote ile ambayo itatokezea wakati wa kumwambia unampenda. Mara nyingi katika situation kama hii mwanamke yeyote ataitikia matakwa yako. Iwapo amekataa usipanic, chukulia ilikuwa tu muda wakujienjoy na kula bata pamoja.

4. Kumuuliza kumtoa out rafiki yako 
Kutoka nje ya 'friend zone' ni jambo moja gumu la kutimiza. Katika hii situation kuna nafasi kubwa ya kupoteza iwapo mwanamke kama huyu atakukataa. Kwanza utapoteza kuwa rafiki yake na pili kama ulikwa unampenda hatakupa nafasi so lazima hapa uwe na umakini wa hali ya juu kwa kila hatua unayotaka kuchukua.
Matokea hapa pia yanaweza kuwa mazuri kwa kuwa unamjua mwanamke kama huyu na pia umemzoea kwa kuwa pamoja kwa muda.

Jambo la kufanya:  Kuwa na nyongo ya kumwambia kuwa unataka kumtoa deti. Weka dhahiri ya kuwa unataka kumtoa dinner. Hawezi kukataa. Kutumia vinywaji na soda haiwezi kumgonga akili yake ya kuwa  una mipango yako, so ni muhimu kuhakikisha unampeleka sehemu ambayo ni romantic na ya kimapenzi.
Ukifanya hivi mwanamke kama huyu ataanza kujaribu kuconnect na wewe na kujaribu kupima kama kuna hisia zozote zile ambazo unajaribu kuonyesha. Kuna nafasi ya kuwa iwapo utampendeza atakukubali kwa uharaka.

Pia weka akilini ya kuwa usitarajie makuu kwani kuna uwezekano mkubwa wa mwanamke kama huyu kukukataa asilani.

5. Kumuuliza kumtoa out mpenzi wako wa zamani
Umeboeka, huna kitu cha kufanya na umeanza kuskiliza nyimbo za Taylor Swift mara ikakujia akilini mwako kuwa unataka kumtoa deti ex wako siku ya valentine?


Chapisha Maoni

0 Maoni