Ujanja unaohitajika hapa ni kuonyesha tenshen ya mapenzi
Kujua kutumia kuleta tenshen ya mapenzi ni jambo kubwa sana mfano wa kuvuna nishati ambayo inaweza kuwapagawisha wanawake kutaka kukutamani pindi unapoongea na wao. Hii ndio maana matumizi ya tenshen ya kimapenzi inafaa itumiwe kwa manufaa mazuri pekee.
Kuna njia tatu kuu ambazo zinafaa kutumiwa kuleta tenshen ya mapenzi:
1. Vile utakavyomuangalia
Jinsi utakavyomuangalia mwanamke kutampa mtazamo wa vile utakavyomfanyia. Ukimuangalia na mtindo fulani wa kimapenzi kutampagawisha papo hapo. Miondoko yako ya macho na mtindo wako wa kuzungumza kutamfanya mwanamke akukubali papo hapo.
2. Toni
Hivi ni vile ambavyo sauti yako inavyopanda na kushuka wakati unapoongea. Hakikisha unatumia sauti ya chini na ya kimvuto, yaani unachukua muda wako kuongea sentensi moja. Amini usiamini ukitumia mtindo wa kusita sita wakati wa kuongea kutamfanya mwanamke kujenga tenshen ya kimapenzi kwako na yeye.
3. Onyesha matamanio yako
Wanaume wengi 'watulivu' wanaogopa kuonyesha matamanio yao kwa mwanamke. Lakini ukweli ni kuwa wanawake hupenda sana kuona mwanamume akionyesha nguvu zake za matamanio lakini hawapendi kuonyesha kama wanapenda jambo hilo. Kuonyesha matamanio yako kwa mwanamke bila kuonyesha azma ya kutaka kitu kutoka kwake ni njia moja wapo ya nguvu yakuleta tenshen ya kimapenzi kutoka kwa mwanamke.
Hebu angalia video fupi ya movie The Aviator Leonardo DiCaprio akitumia mbinu hizi tatu kumtongoza na kumshawishi mwanamke chini ya dakika mbili
Hio tenshen ya kimapenzi umeiona ilivyojitokeza?
Ok najua hii ni scene ambayo imetoka katika movie lakini jambo hili linaweza kujitokeza katika maisha ya kawaida. Leo hapa anaonyesha nguvu zake na confidence yake ya kimapenzi. Mwanaume muoga na asiyejiamini mbele ya wanawake jambo kama hili hangeweza kulifanya kamwe. [Soma: Hatua za kutoa uoga wa kuapproach mwanamke]
Fanya mazoezi ya kujifunza jinsi ya kuleta tenshen ya kimapenzi kwa mwanamke halafu baadaye tutarudia kulifafanua zaidi swala hili zima
0 Maoni